Saturday, December 31, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 4

Volume 4 ndio toleo la mwisho katika awamu hii mpya ya Jifunze Kuimba na Joett Mkito. Fuata maelekezo. Panapokupa taabu, tafadhali niulize nikupe muongozo. Download Vol. 4 hapa!

Ukishaweza hili zoezi la takriban dakika 10, sasa utakua unamazoezi ya sauti Vol. 1, 2, 3 & 4 katika ratiba yako ya kujifunza kuimba. Kwahivyo, kilamara unapo kaa kufanya mazoezi yote haya kwa pamoja, unapaswa kufanya zoezi la pumzi kabla ya Vol. 1 alafu kuendelea na mazoezi ya Vol. 2, 3 & 4 bila ya kusimama. Jumla ya muda wa mazoezi ukiunganisha hizi Volume zote 4 ni dakika 30.

Kumbuka, madhumuni ya haya mazoezi ni ku re-balance sauti yako, au kurekebisha matumizi ya sauti yako ili uweze kuimba kwa urahisi kwenda juu na kwenda chini; na mpangilio na ratiba hii ndio itaweza kukupa wewe huo uwezo kwa njia ya haraka na salama zaidi. Tafadhali usianze kukurupuka na ku-download vitu olela kwenye internet. Tafadhali fuata maelekezo yangu na mazoezi niliokuandalia ili uweze kupata mafanikio ya uhakika.

Nilicho kifanya hapa nikujaribu kuwezesha watanzania wote popote walipo, kupata mafunzo stahiki ya sauti bila ya gharama ya kuhudhuria mafunzo ya sauti darasani pamoja na mimi. Maelekezo na mazoezi haya ni nyeti kwa kukuwezesha kufikia malengo yako. Sikiliza. Tenda. Utapata faida kubwa sana kwenye swala la kuimba. Amini hilo!

RATIBA YA TOLEO Vol. 4, 5, 6 & 7

Joett Vocal Drills Vol. 4 OUT 3.01.2017
Joett Color Me Beautiful Drills Vol. 5 OUT  17.01.2017
Joett Color Me Beautiful Drills Vol. 6 OUT  31.01.2017
Joett Color Me Beautiful w/B Track Vol. 7 OUT 14.02.2017
Joett - Color Me Beautiful (Acoustic Pop)  OUT 28.02.2017

Muongozo wa Mazoezi

Download Mazoezi Mkito.com
Weka kwenye CD au Flash Disk
Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba.
Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2
Volume 1, 2 & 3 Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! Nawatakia mafanikio mema!


JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel
Madarasa ya Studio


No comments:

Post a Comment