Thursday, November 24, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 1

Kwa awamu nyingine tena, na tena safari hii kwa maboresho yalio fuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao, ninawaletea toleo mpya kabisa Jifunze Kuimba na Joett Mkito Volume 1. Hili toleo ni muhimu katika kukuwezesha kuingia katika mstari wa mafunzo ambayo bila shaka, yatakuletea mafanikio ya haraka.

Kabla ya kuanza, hakikisha una download na kufanya zoezi langu la pumzi Mkito.com

Bila ya kuzungumza maneno mengi, nataka niwaachie toleo hili la kwanza (Vol. 1) msikilize mifano nakuendelea na mchanganyiko wa mazoezi ya sauti kwa takriban dakika 8. Mifano ipo. Nikusikiliza tu na kufuata hiyo mifano, na la msingi kabisa nikuachia sauti ifuate mkondo wake. Usilazimishe sauti. Iachie ifuate kinanda na maelekezo mwanana.

Muongozo wa Mazoezi

  • Download mazoezi Mkito.com
  • Weka kwenye CD au Flash Disk
  • Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba. 
  • Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni. 
  • Ku-Download PDF yenye maelekezo ya Volume 1, 2, 3 & 4 Bofya hapa!
  • Kusoma Press Release bofya hapa!

Ukiwa na maswali, jiskie huru kuniuliza, au soma nakala kadhaa nilizo andika:
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio

No comments:

Post a Comment