Sunday, May 19, 2013

Mwalimu wa Kuimba Aachia CD Ya Kujifundishia Kuimba

BUSINESS TIMES WALICHAPA KWA LUGHA YA KIINGEREZA TAREHE 16/5/2013: Jifunze Kuimba na Joett CD Yazinduliwa Joett, mwalimu wa kuimba na jaji katika kipindi cha TIKISA kinachorushwa ITV, ameachia CD ya kujifunzia kuimba ijulikanayo kama Jifunze Kuimba na Joett. Mazoezi hayo ya kuimba ambayo yalianza kurekodiwa mwaka 2010 na kumaliziwa Machi 2013, yanamchipuko wa singo yake I Could Never Live (Without Your Love), ambayo iliachiwa mwaka 2010/2011. Joett aliandaa mafunzo hayo pamoja na mpiga kinanda mahiri Luigi Tamburi, ambae miaka ya nyuma alikua mpiga kindanda wa concert jijini New York, Marekani. Joett, ambae singo yake mpya Color Me Beautiful inamahadhi ya miondoko ya disco la miaka ya 70, alisema, “Nilitaka kuandaa mafunzo ambayo ni kamilifu na yanayotumia irabu pamoja na mashairi kwenye mpangilio wa kujifunza kuimba. Kwa kawaida mafunzo ya kuimba hutumia irabu. Lakini mimi nilitaka kutengeneza mpangilio ambao una mashahiri pia, ili iwe rahisi na haraka zaidi kutumia ujuzi huo kwenye wimbo wowote”. Maelekezo kwenye CD hiyo ni kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

“Naamini huu utakua mchango wangu mkubwa wakukuza vipaji hapa nchini ili vijana wetu waweze kujiendeleza katika fani hii,” alisema Joett. “Kwa kutumia mazoezi haya katika miezi michache iliyopita, nimeweza kurekebisha sauti za wanafunzi wangu kwa urahisi zaidi,” Joett aliongeza.

Kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, Joett huandika ushauri kuhusu maswala ya kuimba kwenye blog lake joettmusic.com, na baada ya kuachia hiyo CD ya kufundishia kuimba tarehe 16 Mei 2013, Joett yuko tayari kusaidia jamii kwa kujibu maswali na kutoa ushauri kuhusu maswala ya uimbaji, kupitia vipindi vya redio na televisheni vya hapa nchini Tanzania.

BUY Learn to Sing with Joett CD Online from TripleClicks

No comments:

Post a Comment